DONALD TRUMP NI MWANAUME SI KAMA PILATO!

DONALD TRUMP NI MWANAUME SI KAMA PILATO!
Usishangae kichwa cha ujumbe huu mfupi ukadhani namaanisha Pontio Pilato, liwali wa Dora ya Waroma hakuwa mwanaume! Alikuwa mwanaume kwa sababu alikuwa akivaa suruali na alikuwa na mke, na watoto! Mkewe tunafahamu alijitokeza wakati wa kesi ya Yesu iliyokuwa ya kutatanisha akamsimulia huyo Pilato mumewe ndoto aliyokuwa ameota usiku.
Usishangae kichwa cha ujumbe huu mfupi ukadhani namaanisha Pontio Pilato, liwali wa Dora ya Waroma hakuwa mwanaume! Alikuwa mwanaume kwa sababu alikuwa akivaa suruali na alikuwa na mke, na watoto! Mkewe tunafahamu alijitokeza wakati wa kesi ya Yesu iliyokuwa ya kutatanisha akamsimulia huyo Pilato mumewe ndoto aliyokuwa ameota usiku.
Huo ni ushahidi kuwa alikuwa mwanaume, lakini uanaume ninaouongelea hapa ni sifa za kiume ambazo Pilato hakuwa nazo! Uanaume ni kuwa na msimamo imara, kutokubabaishwa, uanaume ni ujasiri na ushujaa. Mwanaume ni mpambanaji mwenye kutetea kweli pasipokubabaishwa na kelele, uanaume ni kusimama msitari wa mbele kupambana na hatari kwa ajili ya wale wanaokutegemea.
Akiwa kwenye kiti cha uliwali alikoketishwa kwa lengo la kutetea walioonewa na kuhukumu kwa haki, ikatokea akaletewa kesi ya mtu aliyeshitakiwa kwa husuda/wivu, mtu huyo ni Yesu Kristo aliyekuwa mwenyeji wa mji wa Nazareti ya Galilaya. Baada ya kusikiliza kesi kwa muda, huku kesi hiyo ikizongwa na washitaki waliokwisha kujichukulia sheria mkononi na kumwadhibu kabla hajahukumiwa, Pilato alisikiliza kesi hiyo, wakaletwa mashahidi ambao walitofautiana wao kwa wao kiasi cha kwamba hata kabla mshtakiwa hajajibu lolote, ushahidi wao ulijionesha dhahiri ya kuwa ni uongo wa wazi usio na kifuniko! Wakati mwingine uongo huwa unafanana na ukweli, lakini ushahidi wa mashahidi hawa ulikuwa ni uongo unaofanana na uwongo!
Kwa zaidi ya mara tatu Pilato alisikika akisema haoni hatia yoyote kwa Yesu, kwa mtu asiye na hatia, mahakama ikishatambua na kudhibitisha hilo, mtuhumiwa huachwa huru. Pamoja na Pilato kulijua hili, alishindwa kumwacha huru Yesu kutokana na kelele za washtaki! Pilato akitaka kujifanya mwema kwa watu wenye wivu alijaribu kulitoa jambazi Baraba eti washtaki wa Yesu wachague nani aachiwe huru kati ya Yesu na Baraba, wenye husuda wakachagua Jambazi Baraba aachwe huru na Yesu Mtenda mema auawe na Pilato akaamua hivyo kutokana na shinikizo la watu!
Wale wafuatiliaji wa historia ya taifa la Israeli, wanajua ya kuwa Yerusalemu umekuwa mji wa Israeli tangu kale. Wanajua jinsi ambavyo miaka zaidi ya elfu moja kabla ya kuzaliwa Kristo Mfalme Daudi alianza kuutengeneza na kuwa mji na makao yake makuu. Mji huu kwa jina lingine huitwa mji wa Daudi, na Yesu akauita MJI WA MFALME MKUU.
Lakini mwaka 135BK, Warumi walipigana na Israeli wakashinda, kwa sababu ya hasira walizokuwa nazo Kaisali wa Roma aliyeitwa Hadrian akaamuru taifa la Israeli lifutwe kabisa kwenye ramani, Waisraeli ambao hawakuuawa waliuzwa kama watumwa, wengine wakakimbilia nchi za jirani kama wakimbizi, pia dora ya Roma ilitunga sheria ya kuzuia Myahudi yeyote asiingie katika ardhi ya Israeli. Tangu wakati huo Ardhi ya Israeli ikagawanywa kuwa ya Waarabu!
Mwaka 1948 Israeli ikaundwa tena, umoja wa mataifa (UN) ukaweka mipaka mipya ambapo Israeli ilipewa karibu nusu ya ardhi yake na nusu nyingine ikahesabika kuwa mali ya waarabu! Pamoja na hayo waarabu hawakuridhika wakaweka msimamo wa kushirikiana kuiondoa Israeli katika ramani ya dunia. Mwaka 1948-1949 wakajaribu kuifuta wakashindwa, wakapigwa wao!
Mwaka 1967 wakaja mataifa zaidi ya kumi, wakapigwa na wengi kuangamizwa na Israeli katika vita ya siku sita. Israeli ikajitwalia maeneo iliyotaifishwa ikiwemo YERUSALEMU MAGHARIBI.
Tangu wakati huo mataifa mengi yamekuwa yakipiga kelele kuitaka Israeli iachie eneo hilo wanalodai ni la wapalestina wakati makaburi ya Wafalme wakuu akiwemo Daudi makaburi yao yako huko!
Wasojua ukweli utawasikia wakilaumu Israeli kwa kufuata mkumbo, eti kwa sababu uamuzi wa kugawa mji huo ulifanywa na viongozi wa UN wa wakati huo! Hivi wewe ungejisikiaje iwapo baati mbaya unafungwa jera, ukirudi unakuta ardhi na nyumba yako vimechukuliwa Na jirani yako, unaenda mahakamani kushtaki, hakimu anaamuru nyumba yako na kiwanja chako hicho ugawane Na huyo tapeli!?
Donald Trump ni mmoja wa watu wanaojua ukweli huu. Katika kampeni zake kabla hajawa raisi wa Marekani aliahidi endapo angeingia Ikulu angehamisha ubalozi wa Marekani toka mji wa Tel-aviv kwenda Yerusalemu. Tamko hilo pekee wakati wa kampeni lilizua gumzo! Hatimaye akafanikiwa kuwa raisi, akaendeleza maono yake, na hatimaye siku ya jana alitangaza rasmi kuutambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.
Baada ya tangazo hilo maneno mengi yalisemwa, maandamano yakafanya na waarabu, bila kuchelewa Kikundi cha magaidi wa Palestrina kiitwacho Hamas kikaanzisha mashambulizi kwa Israeli, Umoja wa Ulaya ukaitisha kikao cha dharura kujadili nini kifanyike!
Neno la Mungu aliye hai linasema:
Zaburi 122:6-8
[6]Utakieni Yerusalemu amani;
Na wafanikiwe wakupendao;
[7]Amani na ikae ndani ya kuta zako,
Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
[8]Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu
Niseme sasa, Amani ikae nawe.
Zaburi 122:6-8
[6]Utakieni Yerusalemu amani;
Na wafanikiwe wakupendao;
[7]Amani na ikae ndani ya kuta zako,
Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
[8]Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu
Niseme sasa, Amani ikae nawe.
Mungu na amlinde na kumbariki Donald Trump.
Ni Mimi Alex E. Bubelwa
Ukipenda niite Mu-Israeli namba 3
0758298888
Ukipenda niite Mu-Israeli namba 3
0758298888
No comments