Barakah The Prince sijawahi kuwa na tatizo na Alikiba ilaa...

Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince amesema hajawahi kuwa na tofauti yoyote na Alikiba bali watu tu ndio huwa wanaeneza manen
Muimbaji huyo aliyejitoa katika label ya RockStar4000 ambayo Alikiba ni miongoni mwa
wasimamizi, amelazimika kufunguka hayo baada ya kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Alikiba
wakati kukiwa na tetesi kuwa hawaelewani.
Barakah ambaye anatamba na ngoma ‘Sometimes’ ameiambia E-Newz, EATV kuwa hilo kila mtu
anaweza kulichukuliwa kwa matazamo wake ila yeye hana tofauti na Alikiba kisa kuondoka RockStar4000.
“Sijawahi kuwa na matatizo na Alikiba na sijawahi kufikiria kuwa na matatizo naye, hayo amatatizo
ni midomo tu ya watu wanatengeneza. Kuondoka kwenye kampuni yao ya kazi siyo kwamba na
matatizo nao, hii ni kazi tu naweza nikahama ofisi yoyote” amesema Barakah.
Ameongeza kuwa kila mtu anaweza kuichukulia tofauti lakini yeye huwa anaishi bila kuangalia
amemridhisha nani au kufanya kwa ajili ya nani kwa sababu anajua hayo ndio maisha yake na wapi anataka kufika.ww
No comments