Sitti aongeza siku kuwasaka vijana wa kwenda kuajiriwa Saudia

Kampuni ya Bravo Job Centre Agency Limited ya malkia wa urembo nchini Tanzania, Sitti Mtemvu leo imeendesha zoezi la kufanya usahali kwa vijana wanaohitaji kazi ya udereva huku akiongeza siku moja zaidi ya kufanyika zoezi hilo kutokana na muamko mkubwa wa Watanzania.

BURUDANI

Sitti aongeza siku kuwasaka vijana wa kwenda kuajiriwa Saudia

By  | 

Kampuni ya Bravo Job Centre Agency Limited ya malkia wa urembo nchini Tanzania, Sitti Mtemvu leo imeendesha zoezi la kufanya usahali kwa vijana wanaohitaji kazi ya udereva huku akiongeza siku moja zaidi ya kufanyika zoezi hilo kutokana na muamko mkubwa wa Watanzania.

Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya National Housing Temeke karibu na Uwanja wa mpira waUhuru ambapo watanzania walipata fursa ya kufanya usahili na kuonyesha uwezo wao wa kuendesha magari makubwa.
“Tunaishukuru Kampuni kubwa ya Almarai ya Saudi Arabia kwa kutupa nafasi za kazi watanzania, hii ni fursa nzuri ambayo imekuja kupitia kampuni yetu na kama ambavyo leo umeona jinsi watanzania walivyojitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa, sisi tumeona siku moja haitoshi tumeongeza siku moja ambapo kesho hili zoezi litaendelea ili watanzania wapate nafasi kwasababu bado tuna nafasi nyingi zaidi,”
Sitti amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika usahili kwani nafasi ni nyingi na wanachotakiwa kuwa nacho ni leseni, passport ya kusafiria pamoja na kujua kingereza za mawasiliano.
Pia alisema nafasi nyingine za ajira ambazo watazitoa kwa siku ya kesho ni pamoja na udereva, wauzaji, wapishi wa mahoteli ambapo amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kwani nafasi ni nyingi.

No comments