ERICAH: SITAKI KUOLEWA, NAKULA UJANA



MUUZA nyago kwenye video za wasanii mbalimbali Bongo, Ericah amesema hataki kuolewa kwa sasa, kwa sababu muda wake wa kufanya hivyo haujafika kwani hajamaliza starehe za ujana.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Ericah alisema zaidi ya wanaume watatu walishamtolea barua ili wamuoe lakini aliwatolea nje sababu bado anataka aendelee kufaidi ujana wake, kwa kuamini ndoa itambana maisha yake ya kula bata, kwani atakuwa chini ya maamuzi ya mtu mwingine

Namshukuru Mungu bahati ya kuolewa ninayo, lakini kichwani mwangu siwazi hilo hata kidogo maana kila kwa wakati, naona muda wangu bado, siwezi nikajifosi kufanya kitu ambacho nafsi yangu haijaridhia, nikaenda kumpasua kichwa atakayenioa,” alisema.

No comments