DAAH WAREMBO WA BONGO WAZIDI KUTEKETEA JELA KWA AJILI YA KUSAKA PESA..


Audhia akiwa chini ya ulinzi.
Akisubiri kupandishwa kizimbani.
Mahad kushoto na Ally nao wakisubiri kupandishwa kizimbani.
Mahad kushoto na Ally nao wakisubiri kupandishwa kizimbani.
Wakili Mwandamizi wa TCRA, Johanes Kalungura akifafanua jambo wakati akizungumza na wanahabari baada ya washitakiwa hao kupelekwa rumande.
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Faudhia Abdi na wenzake, Mahad Salat na Ally Yusuf leo (Alhamisi) wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na kusomewa mashitaka sita ya uhujumu uchumi kwa kutoa huduma za simu bila kibali jambo lililoiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 370.
Faudhia na wenzake raia wa Somalia wakiwa mahakamani hapo mbele ya hakimu, Wilbard Mashauri, wakili wa serikali, Jehovanes Zacharia aliwasomea mashitaka sita ya uhujumu uchumi.
Akiwasomea mashitaka yao wakili huyo aliyataka makosa hayo kuwa ni kuingiza nchini vifaa vya kielekroniki kinyume cha sheria, kuunganisha vifaa vya kielekroniki bila kibali, kuendesha shughuli za kielekroniki bila kibali, kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila kibali, kutumia vifaa vya kielekroniki bila leseni kosa la sita ni kuiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 370.
Hata hivyo wakili Jehovanes aliiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo aliiomba mahakama hiyo kupanga siku nyingine ya kusikiliza kesi hiyo.
Kufuatia kesi hiyo kutokuwa na dhamana washitakiwa hao wote watatu wamepelekwa rumande mpaka Desemba 6 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

No comments